Nyota wa Kimataifa wa Simba raia wa Afrika Kusini, Neo Maema, amefunguka kuwa mafanikio ya timu hayategemei mchezaji mmoja pekee, bali mshikamano na umoja wa timu nzima ikiwemoΒ viongozi.
Neo amesisitiza juu ya uwepo wa mshikamano ndio msingi wa safari ya Simba kuelekea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu pamoja na kufanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali.
βUmoja, morali na mshikamano wa timu ndiyo silaha muhimu zaidi. Hizi huchangia kuunda mazingira mazuri ya kushirikiana ndani na nje ya uwanja,β aamesema na ameongeza kuwa hali hiyo inachochea wachezaji kushirikiana kama familia moja.
Kiungo huyo amebainisha kuwa wachezaji wachache wanaweza kuamua matokeo ya mechi fulani, lakini timu yenye mshikamano na umoja ndiyo inayoweza kubeba mataji mwishoni mwa msimu.
Bila kusahauΒ meridianbetΒ ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Aneongeza kuwa mshikamano unazidi mbinu za kucheza pekee, na furaha yake kubwa inatokana na kuona wachezaji wakiwa na mshikamano huo ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo.
βNajua inahitajika nini ili kushinda ligi. Mshikamano ni kiini cha mafanikio,β amesema Maema, amefafanua kuwa furaha iliyopo ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo na namna wachezaji wanavyoshikamana ni jambo muhimu sana kwake.




