Corriere dello Sport inaripoti kuwa Roma wako tayari kushindana na Juventus ili kumsajili beki wa AFC Bournemouth, Marcos Senesi, kama mchezaji huru mwezi Juni.

Beki huyo wa Bournemouth amevutia vilabu vya Serie A, Juventus na Roma.
Gazetta dello Sport iliripoti Ijumaa kuwa Bianconeri wako tayari kumpa beki huyo wa kati wa Argentina mkataba wenye thamani ya zaidi ya euro milioni 4 kwa msimu. Hata hivyo, kwa mujibu wa Corriere dello Sport, timu hiyo pia wanafuatilia kwa karibu hali ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.
Gazeti hilo la jijini Roma limethibitisha kuwa Senesi hataongeza mkataba wake na Bournemouth, na ataondoka katika klabu hiyo ya England kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu.
Hapo awali, Barcelona na Napoli walihusishwa na beki huyo wa Argentina, lakini sasa Roma na Juventus ndio vinatajwa kuwa wagombea wakuu wa kupata saini yake.


