Simba Yachukua Pointi 3 kwa KMC

Ligi kuu ya NBC Tanzania iliendelea hapo jana kwa mechi kadhaa ila mechi ambayo ilikuwa ikisubiriwa kw ahamu ni hii ya KMC dhidi ya Simba SC mchezo ambao ulipigwa majira ya saa 1:00 usiku.

Simba Yachukua Pointi 3 kwa KMC

Mchezo huo ulimalizika kwa Simba kupata mabao 2-0 katika kipindi cha kwanza cha mchezo baada ya Selemani Mwalimu na Libasse Gueye kupachika mabao hayo mazuri kabisa kabla ya mapumziko.

Libasse Gueye huu ni usajili mpya ambao Wekundu wa Msimbazi wameufanya hivi karibuni na kuonekana kuwa na mchezaji mzuri ambaye amekuja kuisaidia timu chini ya kocha mkuu Steve Berker.

KMC ilimaliza mchezo huo wakiwa pungufu baada ya beki wao, Castor Mwangabo kupewa kadi nyekundu na mwamuzi Ahmed Arajiga baada kucheza mchezo usio wa kiungwana.

Meridianbet inakwambia kuwa endelea kubashiri hapa kwani ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000 yapo hapa. Ingia kwenye akaunti yako na uanze safari yako ya ushindi sasa.

Simba Yachukua Pointi 3 kwa KMC

KMC wao chini ya kocha mkuu Mohamed Bares wameendelea kuwa na matokeo mabovu ambayo hayaridhishi kabisa kwenye ligi hadi sasa kwani bado wanashika nafasi ya mwisho wakiwa na pointi zao 8 kwenye michezo 15 ambayo wamecheza.

Simba baada ya ksuhinda jana anaendelea kuwa nafasi ya 6 baada ya michezo 8 ambayo amecheza na kukusanya pointi 19. Mechi ijayo atakuwa nyumbani kukamilisha mechi yake ya makundi kwenye ligi ya mabingwa dhidi ya Stade Malien.

Wakati kwa upande wa KMC wao watakuwa ugenini dhidi ya Singida Black Stars ambao mpaka sasa wapo nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.