Simba SC Yachukua Hatua Kwa Kauli Za Kashfa Dhidi Ya Mo Dewji

Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba SC imelaani vikali vitendo vya baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa wanachama kuitisha mkutano na kutoa kauli za kashfa pamoja na maneno yasiyo na staha dhidi ya Mwekezaji wa Klabu hiyo, Ndugu Mohammed Dewji.

Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na uongozi wa klabu, Simba SC imesema vitendo hivyo havikubaliki na ni kinyume na maadili, heshima na misingi ya klabu hiyo kongwe nchini. Uongozi umeeleza kusikitishwa kwake na matamshi yaliyotolewa, huku ukisisitiza kuwa hayawakilishi misimamo wala maadili ya Simba SC.

Simba SC Yachukua Hatua Kwa Kauli Za Kashfa Dhidi Ya Mo Dewji

Katika hatua nyingine, Bodi ya Wakurugenzi imethibitisha kuwa tayari imelifikisha suala hilo kwa Jeshi la Polisi ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya wote waliohusika moja kwa moja au kwa njia ya kula njama katika mkutano huo. Lengo ni kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake na wahusika wanawajibishwa kwa mujibu wa taratibu za nchi.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Aidha, uongozi wa Simba SC umetoa pole kwa Mwekezaji wake, Mohammed Dewji, kwa kauli na vitendo vilivyolenga kumdhalilisha, huku ukisisitiza kuwa mchango wake kwa klabu na maendeleo ya soka nchini unatambulika na kuheshimiwa.

Simba SC Yachukua Hatua Kwa Kauli Za Kashfa Dhidi Ya Mo Dewji

Bodi ya Wakurugenzi imesisitiza kuwa haitavumilia mtu au kikundi chochote kitakachojaribu kuchafua taswira ya klabu, na imewataka wanachama na mashabiki wa Simba kuendelea kudumisha mshikamano, heshima na umoja kwa maslahi ya klabu.

Hatua hiyo inakuja wakati Simba SC ikiendelea na maandalizi ya michezo yake ya ndani na kimataifa, huku uongozi ukiahidi kuendelea kulinda maslahi ya klabu dhidi ya vitendo vyovyote vinavyoweza kuhatarisha umoja na uthabiti wake.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.