Guardiola Dhidi ya Mikel Arteta Vita Ya Fainali Carabao

Baada ya vijana wa Pep Guardiola, Manchester City kuibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Newcastle United jana usiku, safari ya kuelekea fainali Carabao Cup imekamilika rasmi, fainali sasa ni kati ya Arsenal na Manchester City. Ni pambano litakalokuwa na mvuto wa kihistoria, kwani linawakutanisha kocha na msaidizi wake wa zamani.

Guardiola Dhidi ya Mikel Arteta Vita Ya Fainali Carabao

Mikel Arteta, kocha wa Arsenal, ana nafasi ya kipekee ya kuandika historia. Ikiwa Gunners wataibuka na ushindi, itakuwa taji lao la kwanza ndani ya miaka sita, jambo ambalo mashabiki wamekuwa wakilisubiri kwa hamu na shauku kubwa. Kwa Arteta, si tu ni ushindi wa taji bali ni kuthibitisha ukuaji wake kama kocha mwenye uwezo wa kuongoza timu kubwa.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Pambano hili pia linachukua sura ya kihisabati na kihistoria, kwani Arteta anakutana na Pep Guardiola, kocha aliyekuwa mwalimu wake wa miaka kadhaa Etihad. Ushindi katika fainali hii ni zaidi ya kombe kwani ni pambano la akili, mbinu, na historia kati ya mwanafunzi na mwalimu wake wa zamani.

Guardiola Dhidi ya Mikel Arteta Vita Ya Fainali Carabao

Kwa mashabiki wa Arsenal, ni fursa ya kuona timu yao ikipata heshima ya ushindi wa Carabao Cup, huku Manchester City ikijaribu kudumisha utawala wa Guardiola kwenye mapambano ya taji, ni Arteta dhidi ya Guardiola, mwanafunzi dhidi ya mwalimu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.