Simba Waomba Ulinzi kwa Mangungu Matokeo Mabovu

Hali si shwari Msimbazi kwani Simba SC wamejikuta kwenye mawimbi makali ya maumivu kufuatia mwendelezo wa matokeo yasiyoridhisha kwenye michuano ya kimataifa msimu huu. Droo ya 2-2 dhidi ya ES Tunis jana Uwanja wa Mkapa, ambayo ilizima matumaini ya kusonga mbele Ligi ya Mabingwa Afrika, imeacha maumivu makubwa kwa mashabiki na hasira hizo zikamiminika moja kwa moja kwa uongozi.

Dakika 45 za kwanza ziliwapa Wekundu wa Msimbazi burudani na ndoto za matumaini. Mabao ya Shomari Kapombe (dk 39) na Yusuphu Kagoma (dk 44) yaliwapeleka mapumzikoni Simba wakiwa mbele 2-0. Lakini mpira una dakika 90. Kipindi cha pili, Esperance wakarudi kwa kasi, wakasawazisha kupitia Aboubacar Diakité (dk 64) na Kouceila Boualia (dk 79).

Simba Waomba Ulinzi kwa Mangungu Matokeo Mabovu

Mwisho wa mchezo ukazua vurugu nje ya uwanja. Kundi la mashabiki lilimvamia Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, wakimtaka ajiuzulu kwa kile walichokiita mfululizo wa matokeo mabaya. Hata hivyo, mashabiki wengine walijitokeza kumtetea, wakisisitiza kuwa Mangungu hachezi uwanjani. Tukio hilo lililazimisha menejimenti ya Simba kuomba ulinzi wa Jeshi la Polisi, huku Bodi ya Wakurugenzi ikiomba hatua zichukuliwe dhidi ya waliohusika na fujo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Simba SC waliponeaponea kupoteza mchezo huo baada ya mchezaji wa Esperance, Hamza Jelassi kupiga penalti iliyopaa juu dakika ya 90+4 ya mchezo. Kwa sare hiyo, mnyama ameokota pointi yao ya kwanza baada ya mechi nne, wakiwa wamepoteza mechi tatu za awali dhidi ya Petro de Luanda, Stade Malien na Esperance yenyewe.

Simba Waomba Ulinzi kwa Mangungu Matokeo Mabovu

Sasa macho yote yanaelekezwa Angola, ambako mnyama atakwenda kumenyana na Petro de Luanda kati ya Februari 6 na 8. Kwenye msimamo wa Kundi D, Stade Malien wanaongoza kwa pointi nane, Esperance wana sita, Petro de Luanda tano, huku yeye akisalia mkiani na pointi moja.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.