Buba Jammeh Ampokonya Nafasi Bala Conte Yanga

Kusajiliwa kwa Buba Jammeh kumegeuza mambo kwa Moussa Bala Conte ndani ya Yanga SC ambaye alionyesha kiwango bora kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar, mpaka kutajwa kama mchezaji bora wa fainali. Hata hivyo, mambo yemeenda ndivyo sivyo kwake mara baada ya sajili hii mpya.

Uongozi wa Yanga umemalizia usajili wa Buba Jammeh, raia wa Gambia, ambaye alijiunga na timu hiyo saa chache kabla ya dirisha dogo la Januari 30, 2026 kufungwa. Hii imesababisha kiungo Conte kuhamishwa kwa mkopo kwenda Raja Casablanca ya Morocco, inayofundishwa na kocha wa zamani wa Simba, Fadlu Davids.

Buba Jammeh Ampokonya Nafasi Bala Conte Yanga

Mapendekezo ya kocha wa Yanga, Pedro Goncalves, yalimlazimisha Conte kuachia nafasi ndani ya kikosi cha wachezaji 12 wa kimataifa, kwani uamuzi wa kuleta Buba ulikuwa lazima. Chanzo cha ndani ya Yanga kimethibitisha kuwa Conte tayari amesafiri Morocco kujiweka sawa na kuanza maisha mapya. Mkopo huu wa miezi sita unatarajiwa kufanikisha maendeleo ya mchezaji huyo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Buba Jammeh Ampokonya Nafasi Bala Conte Yanga

Kutua kwa Buba, mwenye umri wa miaka 24, kumeongeza idadi ya wachezaji wa kimataifa Yanga hadi 13, wakati kanuni zinaruhusu 12 tu. Hii ilisababisha uamuzi wa Conte kuondolewa, sawa na aliyoyakabili Andy Boyeli (Sekhukhune) na Mohamed Doumbia (Marumo Gallants), huku Celestine Ecua naye akipelekwa JS Kabylie kwa mkopo.

Buba amewahi kuichezea Interclube ya Angola, ana uwezo wa kucheza winga pande zote, akitumia miguu yote miwili kwa ufasaha, huku akiwa anaweza pia kusimama kama mshambuliaji wa kati.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.