Yanga Watuma Ujumbe Mzito Kwa Simba Kuelekea Derby

Mabingwa wa Kihistoria wa Ligi ya Tanzania Yanga imerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo uliopigwa jana saa 10 katika Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge Dar es Salaam.

Yanga Watuma Ujumbe Mzito Kwa Simba Kuelekea Derby

Katika mchezo huo, mabingwa hao watetezi walionyesha ubora mkubwa kuanzia dakika za mwanzo hadi mwisho wa mchezo, ikitawala umiliki wa mpira na kutengeneza nafasi nyingi za mabao. Ushindi huo umeipa timu hiyo morali kubwa kuelekea michezo ijayo, hususan Kariakoo Derby inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Mohamed Hussein, Laurindo Dilson β€˜Depu’, Mudathir Yahya, Prince Dube na Sheikhan Khamis, kila mmoja akichangia kwa namna yake kuifanya timu hiyo iondoke na alama zote tatu muhimu.

Bila kusahauΒ meridianbetΒ ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Yanga Watuma Ujumbe Mzito Kwa Simba Kuelekea Derby

Kwa matokeo hayo, Yanga imefikisha pointi 28 na kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi sawa na JKT Tanzania waliopo nafasi ya pili. Hata hivyo, Yanga inaongoza kutokana na ubora wa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Ushindi huo si tu umeimarisha nafasi yao juu ya msimamo, bali pia umetuma salamu nzito kwa wapinzani wao kabla ya Kariakoo Derby, huku kikosi hicho kikionekana kuwa katika kiwango bora na tayari kwa mapambano makubwa yanayofuata.

Yanga Watuma Ujumbe Mzito Kwa Simba Kuelekea Derby

Yanga wamesafiri leo kuelekea Zanzibar kwa ajili ya mchezo huo ambao umepangwa kupigwa Machi Mosi New Amani Complex Unguja Zanzibar.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.