Chelsea wameripotiwa kurejea kwenye meza ya mazungumzo kukamilisha uhamisho wa Enzo Fernandez na wanataka kumsajili kiungo huyo wa Benfica kabla ya tarehe ya mwisho ya usajili hapo kesho.

Miamba hao wa Ureno walikataa dau la pauni milioni 70 kwa ajili ya nyota wao wa Kombe la Dunia Muargentina mapema mwezi huu lakini The Blues wako tayari kwenda juu zaidi ili kufanikisha dili hilo.
Kwa mujibu wa gazeti la The Telegraph, West London wametoa mapendekezo mawili mapya ambayo wanatumai kuwa watapata usajili wao wa nane kwenye dirisha la Januari.

Wakuu wa Stamford Bridge wamejitolea kutoa pauni milioni 85 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 na kuruhusu mmoja wa wachezaji wao kujiunga na Benfica kama malipo, huku pia wakiwa tayari kumlipa Fernandez pauni milioni 105 kwa awamu kwa awamu.
Huku Eagles hapo awali wakisisitiza kuwa kipengele chake kinalipwa kikamilifu, inabakia kuonekana ikiwa wanashawishiwa na ofa hizo mpya.

Fernandez anaaminika kutaka kuhamia Chelsea hivyo kukubaliana masuala ya kibinafsi mwishoni mwa dirisha hakutakuwa tatizo.

