Gazeti la Gazzetta dello Sport limearifu kuwa Tottenham Hotspur na Bayern Munich wanaonyesha nia ya kweli ya kumsajili mshambuliaji wa Juventus, Dusan Vlahovic, ambaye kwa sasa anapitia kipindi kigumu.

Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Serbia bado ndiye mfungaji bora wa Juventus msimu huu akiwa na magoli manne katika mechi 11 kwenye mashindano yote, lakini hajafanikiwa kufunga tangu Septemba 16.
Jumapili, alianza katika mchezo uliomalizika kwa Juventus kupoteza 1–0 dhidi ya Lazio, matokeo ambayo yalikuwa kipigo cha tatu mfululizo kwa Bianconeri na yakasababisha kufutwa kazi kwa kocha Igor Tudor.
Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1991, Juventus hawajafunga katika mechi nne mfululizo, na hawajashinda katika mechi nane mfululizo tangu mwaka 2009. Ingawa Tudor alimrithi Thiago Motta mnamo Machi 2025, gazeti hilo limeonya kuwa si sahihi kumlaumu peke yake kwa kuporomoka kwa kiwango cha Juventus hivi karibuni.
Gazzetta pia imeeleza kuwa Juventus wanakosa wachezaji wa kiwango cha juu ndani ya kikosi chao, huku likifanya uchambuzi maalum wa hali ya Vlahovic.



