Ripoti nyingi zinadai nyota wa Italia na PSG Gianluigi Donnarumma alifanyiwa uvamizi na kuibiwa nyumbani kwake huko Paris jana usiku.

Vyombo vya habari vya Ufaransa Actu 17 na vyanzo kadhaa vya kuaminika nchini Italia, vikiwemo ANSA na La Gazzetta dello Sport, viliripoti wezi walivamia nyumba ya Donnarumma katika eneo la VIII mjini Paris jana usiku wakiwa na mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia na mpenzi wake Alessia Elefante wakiwa ndani.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Donnarumma alifungwa kamba na kuvuliwa nguo na wezi waliiba bidhaa zenye thamani ya Euro 500,000.
Gianluig na mpenzi wake walifanikiwa kujikomboa saa 3.20 asubuhi, wakielekea kwenye hoteli ya kifahari karibu na nyumbani kwao.

Mamlaka za eneo hilo ziliarifiwa mara moja na kuwatunza wenzi hao, ambao walilazwa hospitalini kwa uchunguzi wa matibabu.
Kipa huyo alijiunga na PSG kwa uhamisho wa bure kutoka Milan msimu wa joto wa 2021 na anajiandaa kuanza msimu wake wa tatu huko Paris.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amecheza michezo 72 na wababe hao wa Ligue 1 na amecheza mechi 54 za kimataifa akiwa na timu ya taifa ya Italia.

