Lautaro Martínez amepata majeraha ya kuvuta msuli (muscle strain) katika misuli ya soleus ya mguu wake wa kushoto. Jeraha hilo linatarajiwa kumuweka nje ya uwanja kwa takribani mwezi mmoja na linaweza kumkosesha dabi dhidi ya AC Milan.

Inter walitoa taarifa rasmi jana kufuatia vipimo vya kitabibu vilivyofanywa asubuhi kwa mshambuliaji huyo.
Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina alipata maumivu ya misuli ya mguu (calf) wakati wa mechi ya UEFA Champions League dhidi ya Bodø/Glimt na alitolewa kipindi cha pili.
Inter walisema vipimo vilibaini kuwa ana “majeraha ya kuvuta msuli katika soleus ya mguu wake wa kushoto” na kwamba hali yake “itatathminiwa tena wiki ijayo.”
Kwa mujibu wa Sky Sport na Corriere dello Sport, Lautaro atalazimika kukaa nje kwa wiki tatu hadi nne, hali inayomaanisha atakosa dabi dhidi ya Milan itakayochezwa mwishoni mwa wiki ya Machi 8.


