CTA Yakiri Bao Dhidi ya FC Barcelona Halikua Sahihi

Mbio za ubingwa wa La Liga zimechukua sura mpya nje ya uwanja baada ya Kamati ya Waamuzi ya Hispania (CTA) kukiri rasmi kuwa bao la ushindi lililofungwa dhidi ya FC Barcelona halikupaswa kusimama. Katika kipigo cha kushtukiza cha mabao 2-1 dhidi ya Girona FC Februari 16 kwenye Uwanja wa Montilivi, Fran Beltran alifunga bao la dakika ya 86 lililozua hasira kubwa kwa Wacatalunya.

CTA Yakiri Bao Dhidi ya FC Barcelona Halikua Sahihi

Barcelona walilalamika kuwa beki wao Jules Kounde alifanyiwa madhambi kabla ya bao hilo, na sasa madai yao yamethibitishwa. Kupitia taarifa ya pamoja, CTA na Shirikisho la Soka la Hispania (RFEF) walisema kuwa mchezaji wa Girona, Claudio Echeverri, aliyeko kwa mkopo kutoka Manchester City FC, alimkanyaga mlinzi wa Barcelona kabla ya mpira kupelekwa kwa mfungaji.

Kwa mujibu wa uchambuzi huo wa CTA, tukio hilo lilipaswa kuhesabiwa kama faulo kwa mujibu wa Sheria ya 12 ya mchezo (Fouls and Misconduct), ambayo inaeleza kuwa kumkanyaga mpinzani kwa uzembe au nguvu kupita kiasi ni kosa linalostahili adhabu. CTA ilikiri kuwa VAR ilipaswa kuingilia kati kwani lilikuwa kosa la wazi na la dhahiri, na mwamuzi alipaswa kubadili uamuzi wake.

CTA Yakiri Bao Dhidi ya FC Barcelona Halikua Sahihi

Barcelona hawakuacha jambo hilo lipite kimya. Kupitia akaunti zao rasmi za mitandao ya kijamii, klabu hiyo ilichapisha ujumbe wenye kejeli: “Kukubali kosa ni hatua kubwa. Kuliepuka ni hatua inayofuata.” Kauli hiyo ilikuja muda mfupi baada ya RFEF kuthibitisha kuwa bao hilo lilikuwa makosa ya uamuzi.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Siku chache kabla ya tukio hilo, Barcelona walikuwa tayari wamewasilisha malalamiko rasmi dhidi ya RFEF kufuatia maamuzi tata, ikiwemo bao la Pau Cubarsi lililokataliwa katika nusu fainali ya Copa del Rey dhidi ya Atletico Madrid baada ya uhakiki mrefu wa VAR.

CTA Yakiri Bao Dhidi ya FC Barcelona Halikua Sahihi

Kocha Hansi Flick alijaribu kupunguza presha kwa kusema kuwa hakutaka kutumia tukio hilo kama kisingizio, akisisitiza kuwa timu yake haikucheza vizuri siku hiyo. Hata hivyo, winga Raphinha alionekana kuwa mkali zaidi, akidokeza kuwa Barcelona wanaonekana kuchezeshwa kwa viwango tofauti ikilinganishwa na wapinzani wao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.