Klabu ya Wolves wametangaza kuwa Julen Lopetegui atakuwa kocha wao mpya baada ya kutimuliwa kwa Bruno Lage mwezi uliopita kutokana na kuwa na matokeo ambayo hayaridhishi.

Lopetegui mwenye umri wa miaka 56, ana wasifu (CV) ya kuvutia baada ya kufurahia vipindi vya kuinoa Porto, Uhispania, Real Madrid na Sevilla na mwishoni kutimuliwa na klabu hiyo baada ya kupoteza dhidi ya Borussia Dortmund kwenye klabu Bingwa.
Wolves wanatarajia makubwa mengi kutoka kwa kocha huyo na mchezo wake wa kwanza kusimamia utakuwa ni dhidi ya Everton, huku mwenyekiti wa klabu hiyo Jeff Shi akisema kuwa; “Julen ni kocha mkuu, mwenye uzoefu bora katika kiwango cha wasomi wa mchezo, na tunafurahi sana kukubaliana na mpango wa kumleta klabuni hapa.”

Aliongeza kwa kusema kuwa tangu mwanzo kocha huyo amekuwa chaguo lao namba moja kuinoa Wolve na wanatazamia kumkaribisha yeye na timu yake watakapoungana nae siku zijazo.
Mafanikio makubwa zaidi ya Lopetegui kufikia sasa yalikuwa ni kunyanyua Ligi ya Europa akiwa na Sevilla mnamo 2019-20, lakini alifukuzwa kazi yake ya usimamizi katika kikosi cha Andalucian mapema msimu huu baada ya kuanza kwa kampeni vibaya.

Sasa, atachukua changamoto mpya akiwa na Wolves ya Uingereza timu ambayo inasuasua kupata matokeo ya kueleweka na sasa ipo nafasi ya 19 kwenye msimamo wa Ligi kuu ya Uingereza.

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.
BONYEZA HAPA

