Mchezaji wa Ligi Kuu ya Uingereza ambaye ameachiliwa kwa dhamana baada ya kukamatwa kwa madai ya ubakaji atastahili kucheza Kombe la Dunia nchini Qatar.

Mchezaji huyo hajafunguliwa mashtaka na ingawa hawezi kutajwa jina lake kwa sababu za kisheria, Athletic wanadai kuwa anatarajiwa kuingia katika orodha ya mwisho ya kikosi cha nchi yake, huku timu zikilazimika kutaja vikosi vyao vya wachezaji 26 ifikapo Novemba 14. Mchezaji huyo ambaye hakutajwa jina alikamatwa mwezi Julai kwa tuhuma za ubakaji.

 

Mchezaji Aliyehusishwa kwa Ubakaji, Aruhusiwa Kucheza WC 2022

Kukamatwa kwa uchunguzi kulikuja huku kukiwa na madai ya matukio mengine mawili dhidi ya wanawake tofauti lakini hakuna mashtaka yoyote yaliyoletwa. Dhamana ya mchezaji huyo iliongezwa mapema mwezi uliopita.

Inaelezwa kuwa taifa lake lilikuwa halifahamu suala lolote linalomhusu mchezaji wao na hivyo wanatazamiwa kuendelea mbele na kumchagua.

 

Mchezaji Aliyehusishwa kwa Ubakaji, Aruhusiwa Kucheza WC 2022

Zikiwa zimesalia siku 10 kabla ya vikosi vya mwisho kuthibitishwa na FAs za timu ya taifa, bado haijafahamika iwapo waandaaji wa mashindano hayo au FIFA wataingilia kati.

Michuano ya Kombe la Dunia itaanza Novemba 20 wakati wenyeji Qatar watakapomenyana na Ecuador. Michuano hiyo inafanyika Mashariki ya Kati kwa mara ya kwanza na itashuhudia timu 32 zikichuana kujaribu kutinga fainali Desemba 18.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa