Viongozi wa klabu ya Simba SC kwa kushirikiana na Kamati ya Maendeleo ya Bunju (Mo Simba Arena) leo wametembelea uwanja huo kuangalia maendeleo ya ujenzi wa ukuta kuzunguka eneo hilo.
“Niwahakikishie wapenzi wa klabu na mashabiki wa Simba, kila senti waliyoitoa inaendelea kutumika kwa maendeleo ya klabu, pamoja na fungu lililoahidiwa kutolewa na mwekezaji mwenza wa klabu yetu, Mohammed Dewji”-Murtaza Mangungu
Simba wapo kwenye hatua ya kuweka ukuta kuzunguka uwanja wao, kabla ya mipango mingine ya kuutanua na kuuongezea sehemu ya mashabiki kukaa.
Kwa upande wa mwenyekiti wa klabu hiyo Murtaza Mangungu, alizungumzia ujenzi huo unavyoendelea alisema kuwa ujenzi umefikia asilimia 70.
Kamati ya Maendeleo ya Bunju (Mo Simba Arena) leo imetembelea uwanja kuangalia maendeleo ya ujenzi wa ukuta kuzunguka eneo hilo. (1)#NguvuMoja pic.twitter.com/1K7mtHyOdI
— Simba Sports Club (@SimbaSCTanzania) November 5, 2022
Mwanzoni mwa mwaka huu wa 2022, klabu ya Simba ilianzisha utarataibu wa kukusanya michango kutoka kwa mashabiki, na wapenzi wa soka ili kusaidia shughuli za ujenzi wa uwanja wa MO Simba Arena, ili uweze kuwa na uwezo wa kutumiuka kwenye mechi za timu hiyo kama uwanja wa nyumbani.
Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.