Ligi kuu ya NBC inaendelea hii leo kwa michezo miwili, ambapo mchezo unaopigwa katika uwanja wa Liti CCM Kirumba majira ya saa 10:00 jioni ambapo Singida Big Stars atakipiga dhidi ya Namungo.

Singida ambaye yupo nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi baada ya kushinda mechi zake saba, amecheza michezo 13 sare tatu na amepoteza michezo mitatu pekee huku leo akiwa nyumbani akitarajia pointi tatu.
Wakati kwa upande wa Namungo wao bado wanashikilia nafasi ya nane baada ya kucheza michezo 13, ushindi mara tano, sare tatu na kupoteza michezo mitano pointi 18 wamejikusanyia kibindoni hadi sasa.

Ushindi wa Namungo hii leo utamfanya apae hadi nafasi ya tano, japokuwa anakutana na Singida ambao sio rahisi kufungwa hivyo wanatarajiwa kina Lusajo watafanya nini katika eneo la ushambuliaji.

