Erik ten Hag ametoa jibu lisiloeleweka alipoulizwa ni lini Jadon Sancho atarejea Manchester United lakini akasisitiza Aaron Wan-Bissaka ana mustakabali katika klabu hiyo.

Sancho aliichezea United mara ya mwisho Oktoba 22 katika sare ya 1-1 dhidi ya Chelsea na aliondolewa kwenye kikosi cha Uingereza kilichoshiriki Kombe la Dunia.
Winga huyo hakusafiri na kikosi kwa ajili ya kambi ya mazoezi ya hali ya hewa ya joto nchini Uhispania wakati wa mapumziko ya nyumbani kwa Qatar 2022 pia, badala yake aliwekwa kwenye programu ya kibinafsi kufanyia mazoezi ya utimamu wake.
United walirejea uwanjani Jumatano katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Burnley kwenye Kombe la EFL na kocha Ten Hag aliulizwa kama anajua ni lini Sancho angepatikana na Sky Sports, ambapo alijibu tu: “Hapana.”

Akibanwa ikiwa kuna ratiba ya kurejea uwanjani kwa nyota huyo wa zamani wa Borussia Dortmund, Ten Hag alitoa jibu lile lile, hata hivyo, alitoa jibu refu zaidi kwa maswali kuhusu Wan-Bissaka, ambaye amekuwa na majeraha msimu huu.
Beki huyo wa pembeni alimtengenezea Christian Eriksen bao la kwanza la United, kabla ya Marcus Rashford kuiwezesha United kutinga hatua ya nane bora.
Wan-Bissaka amekuwa na matatizo ya kuwa na uthabiti tangu alipowasili kutoka Crystal Palace mwaka wa 2019 na amekuwa akihusishwa na kurejea Eagles. Ten Hag, hata hivyo, anasema beki huyo anaweza kuwa na nafasi Old Trafford.

Ten Hag; “Aaron Wan-Bissaka, ni wazi ana mustakabali, amekuwa na miaka mizuri na United, lakini tangu mwanzoni mwa msimu huu alikuwa na magonjwa mengi na majeraha”

