KMC Yaendeleza Ilipoishia, Yavuna Pointi 3

Klabu ya KMC imeanza kurejea kwenye ubora wake kwenye Ligi kuu ya NBC baada ya kumtwanga Polisi Tanzania kwa mabao 2-0 katika uwanja wa Uhuru katika mchezo wa mapema hii leo.

 

KMC Yaendeleza Ilipoishia, Yavuna Pointi 3

KMC wameshinda mchezo huo wa pili mfululizo ambapo mabao yao yamefungwa na Awesu Ally mapema kabisa dakika ya 06 kabla ya George Makang’a kupachika bao la kujihakikishia ushindi dakika ya 55.

Baada ya ushindi huu wa leo KMC wanasogea hadi nafasi ya 8 kwa kujikusanyia pointi 22 huku Polisi Tanzania wao wakizidi kusalia mkiani kwenye msimamo wa Ligi wakiwa na pointi zao 9.

Polisi baada ya kupoteza mechi hii mchezo unaofuata watakuwa nyumbani kuwaalika Coastal Union ambaye nae katoka kupoteza na mchezo huo atahitaji matokeo ajiweke kwenye nafasi nzuri.

KMC Yaendeleza Ilipoishia, Yavuna Pointi 3

Wakati Wanakino Boys mchezo wao unaokuja watamenyana dhidi ya Simba tarehe 26 huko CCM Kirumba wakikumbuka mechi ya kwanza walitoa sare, wanakutana na mnyama ambaye amedondosha alama dhidi ya Kagera Sugar.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.