Ligi kuu Tanzania Bara kuendelea hii leo kwa michezo miwili ambapo mchezo wa mapema ni wa Mbeya City dhidi ya Mtibwa unaopigwa majira ya saa 10:00 jioni.

Mbeya City wapo nafasi ya 11 baada ya michezo 20, wakiwa wameshinda mechi zao nne, sare tisa na kupoteza jumla ya michezo saba hadi sasa huku wakivuna pointi zao 21 wakiwa wamepoteza mechi tatu mfululizo.
Wakati kwa upande wa Mtibwa Sugar wao wapo nafasi ya nane baada ya michezo 20, wakiwa wameshinda michezo yao sita, sare saba na kupoteza michezo yao saba wakiwa wamejikusanyia pointi 25.

Mtibwa wao mechi tano za mwisho hakuna hata moja ambayo wamepata pointi tatu, wametoa sare tatu na kupoteza michezo miwili. Leo hii wapo ugenini wakihitaji ushindi ili wavuke nafasi ya nane je wataweza mbele ya Wanakoma Kumwanya?

