Klabu ya Yanga ambayo ipo chini ya kocha mkuu Nasredinne Nabi inazidi kuusogelea ubingwa baada ya kuitungua Namungo mabao 2-0 katika dimba la Mkapa kwenye mchezo uliopigwa jana.

Mabao hayo ya kuipatia Yanga pointi 3 yalitupiwa kimyani na beki wao wa kati Dickson Job na bao la pili lilipachikwa na Stephan Aziz Ki baada ya mlinda mlango wa Wauaji wa Kusini kutoa boko lililomkuta kiungo huyo na kutupiwa bao kambani.
Hivyo baada ya ushindi huo Young Africans wanazidi kujikita kileleni wakiwa na pointi 59, mbele kwa pointi 6 kwa anayemfuata ambaye ni Simba. Na timu hiyo imeshinda mechi zake 9 mfululizo.

Namungo kwenye mechi tano alizomenyana dhidi ya Yanga hajashinda hata mchezo mmoja na vijana wa Nabi wamekuwa ni wababe wa timu hiyo toka wapande ligi kuu msimu wa 2019.
Baada ya kupoteza mchezo huo amebaki nafasi ya sita akiwa na pointi zake 29 kwenye msimamo wa ligi.

