Kiungo wa kati wa Chelsea Tiemoue Bakayoko ameachiliwa baada ya kumalizika kwa mkataba wake, klabu hiyo imethibitisha.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alisajiliwa na meneja wa zamani Antonio Conte muda mfupi baada ya timu hiyo kunyakua taji la Ligi Kuu ya Uingereza mwaka 2017 lakini alikuwa hajaichezea klabu hiyo tangu mwisho wa msimu wake wa kwanza.
Tangu wakati huo amekuwa kwa mkopo AC Milan ambaye alishinda naye taji la Serie A mnamo 2022 Napoli na klabu ya zamani ya Monaco.
Aliwasili Stamford Bridge kwa ada ya pauni milioni 40 baada ya kuisaidia Monaco kunyakua ubingwa wa Ligue 1 kwa mshangao, baada ya kuwa sehemu ya timu iliyowajumuisha Kylian Mbappe na Bernardo Silva.

Kikosi hicho kinachonolewa na Leonardo Jardin kiliiondoa Manchester City katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kuelekea kufuzu kwa nusu fainali dhidi ya Juventus.
Lakini kiungo huyo, ambaye aliichezea Ufaransa mechi moja mwaka 2017, alishindwa kutimiza matarajio yaliyoambatana na ujio wake.
Wakati wake wa kukumbukwa zaidi akiwa na rangi ya samawati ulikuja wakati wa fainali ya Kombe la FA 2018 alipocheza kwa dakika 90 wakati kikosi cha Conte kilishinda washindi 1-0 dhidi ya Manchester United na kubeba kombe hilo.

Wachezaji wengine 12 waliotoka katika akademi ya Chelsea pia wameondoka katika klabu hiyo kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na Ligi kuu, akiwemo mlinda mlango Nathan Baxter ambaye alicheza mara 12 kwenye Championship kwa mkopo Hull msimu uliopita.

