Konate Kuondoka Liver Msimu Huu

Kwa mujibu wa ripoti kutoka The Athletic, mazungumzo ya mkataba kati ya Ibrahima Konaté (26) na Liverpool bado hayajafikia mafanikio yoyote.

Konate Kuondoka Liver Msimu Huu

Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa kwa sasa yuko huru kuanza mazungumzo ya awali ya mkataba (pre-contract) na klabu zilizo nje ya Ligi Kuu Uingereza,  huku mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Mabingwa wa Ligi Kuu England wameweka wazi nia yao ya kumbakiza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 katika dimba la Anfield. Hata hivyo, licha ya Liverpool kuwasilisha mapendekezo matatu ya mikataba hadi sasa, beki huyo wa zamani wa RB Leipzig bado hajakubali makubaliano yatakayomuwezesha kubaki Merseyside. Klabu za Real Madrid na Paris Saint-Germain zimekuwa zikihusishwa na mpango wa kumsajili mchezaji huyo wa Ufaransa.

Kutokana na hali ya sintofahamu kuhusu mustakabali wa Konaté, The Athletic inaeleza kuwa Liverpool wameelekeza nguvu zao katika kutafuta beki mpya wa kati wakati wa dirisha la usajili wa majira ya kiangazi. Aidha, mikataba ya Virgil van Dijk na Joe Gomez inatarajiwa pia kumalizika katika majira ya kiangazi ya mwaka 2027.

Konate Kuondoka Liver Msimu Huu

Liverpool mpaka sasa wapo nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi wakikusanya pointi zao 36 baada ya kushinda mechi 10, sare 6 na kupoteza mara 5 hadi sasa. Je vijana hao wa Slot watamaliza nafasi ya ngapi?

Meridianbet wanakwambia kuwa ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000 yapo hapa kwenye mechi za leo. Ingia na ubashiri leo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.