Klabu ya Nottingham Forest imemtimua aliyekuwa kocha wao Sean Dyche baada ya kuwa na matokeo mabaya kwenye ligi na hii ikiwa ni mechi ya 3 hajashinda.

Forest walikuwa nyumbani jana kumkaribisha Wolves ambao ni vibonde wa ligi huku uongozi ukitarajia ushindi kwenye mchi hii lakini mechi iliisha kwa wenyeji hao kupata suluhu.
Sean Dyche anakuwa ni kocha wa 3 msimu huu kufukuzwa klabuni hapo baada ya Nuno Santos na Ange Postecoglu ambao waliondolewa klabu hapo kutokana sababu mbalimbali.
Ikumbukwe kuwa Nottingham chini ya Nuno ilikuwa ni moja ya klabu tishio kweye ligi kwani waliweza kumaliza nafasi ya 7 ambayo iliwafanya washiriki michuano ya Europa Barani Ulaya.
Hivyo baada ya kumfukuza Dyche sasa wanajiandaa kusaka kocha mpya ambaye ataleta mabadiliko klabuni hapo ukizingatia kuwa wapo kwenye michuano ya Europa League.

Meridianbet inakwambia kuwa endelea kubashiri hapa kwani ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000 yapo hapa. Ingia kwenye akaunti yako na uanze safari yako ya ushindi sasa.
Dyche ameduma klabu hapo miezi 4 pekee na ameiacha timu ikiwa nafasi ya 17 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi zao 27 kwenye mechi 26 ambazo wamecheza.

