Arsenal ya Gyokeres walitoa majibu bora kabisa baada ya kutoka sare na timu ya mkiani mwa Ligi Kuu wiki iliyopita waliwachapa mahasimu wao wakubwa Tottenham kwa mabao 4-1 ugenini na kuzuia, angalau kwa sasa, kuporomoka tena baada ya kuwa wanaongoza msimamo wa ligi.

Sehemu ya mafanikio hayo ilitokana na mkutano wa kikosi uliokuwa na “moto”, kama Gyokeres alivyofichua.
Gyokeres ambaye ni raia wa Uswizi, aliyefunga mabao mawili katika dabi ya London, alieleza jinsi mazungumzo kati ya wachezaji yalivyokuwa na athari na yalihusisha karibu kikosi kizima.
“Nadhani wengi wetu tulizungumza na naamini ni muhimu wakati mwingine kusema unachohisi na kukitoa hadharani ndani ya kundi ili kila mmoja aelewe jinsi wengine wanavyohisi wakati huo. Unapata uelewa mzuri zaidi wa hisia za kila mmoja na unapozungumza waziwazi ndani ya kundi, naamini mnakuwa karibu zaidi, na hilo ni jambo muhimu sana kufanya wakati mwingine.” Alisema Gyokeres
Kama huna uaminifu, nadhani ni vigumu kuboresha. Ilikuwa mazungumzo mazuri, hakika tumefurahia leo, na sasa tutajipanga kwa ajili ya mchezo mkubwa dhidi ya Chelsea wikiendi ijayo.

Gyokeres pia alirejea sare ya kuumiza dhidi ya Wolves, iliyothibitishwa katika dakika za nyongeza za kipindi cha pili. Daima itakuwa vigumu unapopata matokeo kama tuliyopata Wolves, lakini ni jinsi unavyokabiliana nayo na jinsi unavyojibu, na leo tumeonyesha hilo kwa njia nzuri. Kupata matokeo na kiwango hiki cha uchezaji, ilikuwa njia kamili ya kujibu. Alisema mchezaji huyo.
Declan Rice tayari alikuwa amezungumzia mkutano wa kikosi siku mbili kabla ya mechi dhidi ya Spurs, kujadili matokeo ambayo yangewaacha Manchester City wakiwa pointi mbili tu nyuma ya vinara kama wangeshinda mchezo wao wa mkononi dhidi ya Crystal Palace.
“Tulizungumza kwa ukali baada ya Wolves, tulijua tumewaangusha sisi wenyewe na mashabiki baada ya kuwa katika nafasi nzuri sana .Kuruhusu ipotee si viwango tulivyojiwekea msimu huu. Tulikuwa na mkutano wa timu na sasa tuko tayari kuanza tena”. Rice aliiambia The Sun


