Arne Slot yuko tayari kuondoka Liverpool, Kwa mujibu wa chanzo cha ndani Indy Kaila, kocha huyo amejiandaa kujiuzulu mwishoni mwa msimu.

Slot amekuwa chini ya presha kubwa hivi karibuni Liverpool. Baada ya kushinda EPL katika msimu wake wa kwanza, kuwa nyuma kwa pointi 21 huku mechi saba zikiwa zimesalia si matokeo mazuri msimu huu.
Liverpool pia walipigwa vibaya kwenye robo fainali ya FA Cup na Manchester City, katika mechi ambayo ilionekana walikata tamaa. Ingawa wako robo fainali ya UEFA Champions League, watakuwa na kazi ngumu dhidi ya mabingwa watetezi Paris Saint-Germain leo hii.
Iwapo watatolewa, Liverpool watabaki bila kitu cha kupigania msimu huu na presha itaongezeka zaidi kwa Slot.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa kocha huyo tayari amejiandaa kuchukua uamuzi wa kuondoka mwenyewe, akitoa ofa ya kujiuzulu mwishoni mwa msimu ikiwa makubaliano sahihi yatafikiwa.
Slot ana mkataba hadi 2027, hivyo fidia haitakuwa kubwa sana iwapo klabu itaamua kuachana naye.
Ripoti nyingi pia zinaeleza kuwa kiungo wa zamani wa Liverpool, Xabi Alonso, anasubiri nafasi ya kuichukua timu hiyo baada ya kuondoka Real Madrid.


