Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba Clatous Chota Chama amefunguka sababu kubwa ambayo imefanya wapotee msimu huu na kusababisha wakose kila kitu.
Chama ambaye anawania tuzo kadhaa msimu huu amesema moja ya kitu kilichowaumiza katika msimu huu unaoenda ukingoni walikua wakifanya mabadiliko katika kikosi chao na kupelekea kukosa uwiano mzuri.
Chama alisema ni jambo baya sana kwao ingawa huwa inatokea kwenye mpira: “Msimu unakwenda ukingoni na tupo tunafanya maandalizi ya mechi za mwisho. Kuhusu kufanya vibaya msimu huu ni mabadiliko ya kikosi mara kwa mara.”
Kocha alikuwa anafanya ‘rotation’ nafikiri hiyo ilikuwa sababu ya kuwa na matokeo ya kubadilikabadilika kwa kuwa tulikuwa tunakosa uwiano. Alisema Cloutus.