Kocha USM Alger Alia na Refa

 

Kocha wa Klabu ya USM Alger Abdul Benchikha alisema wazi kuwa licha ya kuwa timu yake kupata ushindi wa mabao 2-1 ugenini mbele ya Yanga, ila kuna vitu hakuridhishwa navyo.

 

Kocha USM Alger Alia na Refa

Benchikha alisema mwamuzi alikuwa bora mwanzoni mwa mchezo huo, lakini kipindi cha pili akabadilika na kuamua kuwa upande wa Yanga kwenye baadhi ya matukio.

“Kipindi cha pili mechi haikuwa nzuri upande wetu kwa sababu hata refa nae akaanza kuonekana kupendelea timu ya nyumbani, hii ni kawaida ukicheza ugenini.”

Kocha huyo aliendelea kusema pia lakini amecheza dhidi ya timu nzuri yenye wachezaji wenye vipaji kuanzia nafasi ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji.

Kocha USM Alger Alia na Refa

Tunarudi Algeria lakini bado mechi haijaisha, ni asilimia 50 kwa 50. Bado tuna kazi ya kufanya Algeria kwa sababu katika mechi ya marudiano Yanga hawana cha kupoteza Watacheza wanavyojua ili wapate matokeo. Alisema kocha huyo.

Acha ujumbe