Juma Mgunda Hajamalizana na Simba Bado

Upo uwezekano mkubwa wa Simba kuendelea na kocha wake msaidizi, Juma Mgunda katika msimu ujao licha ya usiri mkubwa ulikuwepo kati yake na mabosi wa timu hiyo.  Mgunda hakuwakatika msafara wa timu hiyo, uliosafiri kwenda nchini Uturuki kwa ajili ya kambi ya wiki tatu kujiandaa na msimu ujao.

 

Juma Mgunda Hajamalizana na Simba Bado

Kocha huyo mzee wa ball itembee ni shuhuda Yanga ikiwa nafasi ya kwanza na kutwaa ubingwa msimu wa 2022/23.

Ni kati ya makocha waliounda benchi la ufundi la Simba lililoifikisha timu hiyo Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita akiwa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ raia wa Brazil.

Habari zimeeleza kuwa uongozi wa Simba hivi sasa unaangalia nafasi nyingine mpya ya kumpa kati ya hizo ni Kocha Mkuu wa Timu ya Wanawake, kama wakifikia muafaka mzuri. Kiliongeza kuwa, Mgunda yeye bado hajaamua hatima yake ya kuchukua nafasi hiyo, lakini taarifa zilizopo kocha huyo anataka kurejea Coastal Union ya Tanga.

Juma Mgunda Hajamalizana na Simba BadoMgunda hatakuwa sehemu ya viongozi ya benchi la ufundi, kwani yapo mazungumzo yanayoendelea kati yake na uongozi wa Simba kujadiliana baadhi ya vitu kuelekea msimu ujao.

Uongozi unahitaji kuendelea na Mgunda kwa nafasi nyingine katika timu, kati ya hizo kuwa Kocha Mkuu wa timu ya Wanawake ya Simba.

“Lakini yeye anaonekana kutohitaji kuwa katika nafasi hiyo, bado mazungumzo yanaendelea kati yake na uongozi,” kilisema chanzo hicho.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alizungumzia hilo kwa kusema: Mgunda hatokuwa sehemu ya benchi la ufundi la timu wakati tutakapokuwepo Tunisia, kwani yeye amebaki kwa ajili ya kushughulikia mambo yake.

Acha ujumbe