Ubabe wa Azam FC kwa Singida FG Ulikuwa Hivi

Azam FC ni washindi wa tatu katika Ngao ya Jamii 2023 baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 Singida Fountain Gate katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

 

Ubabe wa Azam FC kwa Singida FG Ulikuwa Hivi

Singida Fountain Gate walikosa utulivu katika kipindi cha kwanza eneo la ulinzi jambo lililowafanya Azam FC kuwatuliza kwa bao la mapema zaidi.

Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.

Ni Prince Dube alianza kumtungua mlinda mlango wa Singida Fountain Gate Beno Kakolanya dakika ya kwanza ikiwa ni muda mfupi baada ya mchezo kuanza.
Wakati Singida Fountain Gate wanapambana kutafuta bao la kuweka usawa nyota Abdul Suleiman, (Sopu) aliongeza chuma cha pili dakika ya 43 ukiwa ni mzigo mzito kwa wapinzani wao.

Ubabe wa Azam FC kwa Singida FG Ulikuwa Hivi

Jitihada za Francis Kazadi, Michael Chuku kwenye kuliandama lango la Azam FC zilikwama kutokana na ukuta imara uliokuwa ukiongozwa na Daniel Amoah kwa Azam FC.

Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.

Eneo la kiungo James Akamiko aliendeleza balaa lake huku kiungo Feisal Salum majaribio yake kadhaa akiwa nje kidogo ya 18 yakiwa ni miongoni mwa yaliyompa tabu Kakolanya wa Singida Fountain Gate.

Ubabe wa Azam FC kwa Singida FG Ulikuwa Hivi

Ikumbukwe kwamba Azam FC iliondolewa katika nusu fainali ya kwanza kwa kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Yanga iliyotinga fainali huku Singida Fountain Gate wao waliondolewa kwa penali 4-2 dhidi ya Simba.

Ukiwa na meridianbet odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti.

Ipo wazi kuwa taji la Ngao ya Jamii 2023 ni mali ya Simba walioshinda kwa penalti 3-1 dhidi ya Yanga kwenye fainali Agosti 13 baada ya dakika 90 kutokufungana.

Acha ujumbe