Chivu: "Inter Hawakuwa na Ushindani wa Kutosha, Lakini Bodo/Glimt Walikuwa na Nguvu Zaidi"

Cristian Chivu ameeleza kuwa Bodo/Glimt “walikuwa na nguvu zaidi” kuliko Inter, akibainisha kuwa wapinzani wao wanaangazia tu Ligi ya Mabingwa, lakini pia amekiri kuwa Nerazzurri hawakuwa na ushindani wa kutosha barani Ulaya.

Chivu: "Inter Hawakuwa na Ushindani wa Kutosha, Lakini Bodo/Glimt Walikuwa na Nguvu Zaidi"

Ilikuwa tayari ni mlima mrefu kupanda baada ya kichapo cha 3-1 katika mechi ya kwanza nchini Norway, lakini hakukuwa na visingizio kuhusu uwanja wa nyasi bandia baada ya kupoteza 2-1 nyumbani katika Uwanja wa San Siro.

Kutokuwepo kwa Lautaro Martinez na Hakan Calhanoglu kulionekana wazi, kwani Inter walikosa makali safu ya ushambuliaji licha ya kutawala mchezo na kupata nafasi kadhaa.

Kosa kubwa la Manuel Akanji lililomruhusu Jens-Petter Hauge kufunga bao la kwanza liligeuka kuwa hatua ya mabadiliko, huku Bodo/Glimt wakiongeza bao la pili kupitia Hakon Evjen, na jaribio la Alessandro Bastoni kwa mpira wa kona likiwa ni la kuchelewa mno.

Chivu alisema: “Tulijaribu kila kitu tangu mwanzo. Tulikuwa tunakutana na timu iliyopangwa vizuri sana, iliyocheza kwa kujilinda kwa wachezaji 10-11 nyuma ya mpira. Labda kushindwa kufungua ukurasa wa mabao mapema kuliwapa utulivu wa kisaikolojia, wakijua tunahitaji mabao mawili kufikisha muda wa nyongeza.”

Chivu: "Inter Hawakuwa na Ushindani wa Kutosha, Lakini Bodo/Glimt Walikuwa na Nguvu Zaidi"

Bodo/Glimt sasa wamepata ushindi wa nne mfululizo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Inter, Atletico Madrid na Manchester City. Inafaa pia kutambua kuwa ligi yao iko mapumzikoni, hivyo tangu katikati ya Septemba wamecheza mechi katika mashindano haya pekee.

“Sina cha kuwalaumu wachezaji wangu, walitoa kila kitu kwa nguvu walizokuwa nazo, lakini kipindi cha pili Bodo walikuwa na nguvu zaidi kuliko sisi,” aliendelea Chivu.

Kuna masikitiko makubwa, kwa sababu tulikutana na timu yenye nguvu zaidi, iliyopangwa vizuri na iliyojua ilichotakiwa kufanya baada ya ushindi wa 3-1 katika mechi ya kwanza, na walitekeleza hilo kwa ustadi mkubwa. Tunaweza tu kuwapongeza Bodo/Glimt, wanastahili kufika raundi inayofuata. Alisema Chivu.

Inter walikuwa wamefika fainali ya Ligi ya Mabingwa mara mbili ndani ya miaka mitatu chini ya Simone Inzaghi, lakini hawakuwa wametolewa mapema hivi tangu Antonio Conte aliposhindwa kuvuka hatua ya makundi msimu wa 2020-21. Safari hii, mfumo mpya wa mashindano unamaanisha safari yao ya Ulaya inaishia hapa.

Chivu: "Inter Hawakuwa na Ushindani wa Kutosha, Lakini Bodo/Glimt Walikuwa na Nguvu Zaidi"

“Lengo letu lilikuwa kuwa na ushindani, na hatukuwahi kufikiria mbali kuhusu mambo tusiyoweza kuyadhibiti,”aliongeza Chivu.

Akizungumzia kasi ndogo ya mchezo, Chivu alisema walijaribu kuzungusha mpira kwa haraka zaidi na kutumia pasi za pembeni kuvunja mfumo wa 4-4-2 wa wapinzani wao, lakini hawakupata pasi ya mwisho sahihi au kushinda walinzi wao katika maeneo ya hatari.

Inter bado wanaongoza Serie A kwa pointi 10 na wanatarajiwa kukutana na Como katika nusu fainali ya Coppa Italia, lakini ilionekana msimu huu walielekeza nguvu zaidi katika malengo hayo kuliko Ligi ya Mabingwa.

Kocha huyo amesme akuwa ni vigumu kupata nguvu unapocheza kila baada ya siku tatu. Na hawezi kuomba zaidi kutoka kwa wachezaji wake kwani walijitahidi kila kitu. Kama wangefunga mapema, huenda hali ingekuwa tofauti, lakini ilikuwa vigumu sana walipokuwa wakijilinda kwa wachezaji 10.

“Tuna huzuni kubwa kwa sababu tulitaka angalau kuwa na ushindani barani Ulaya, lakini tulikutana na timu iliyocheza mechi nne tu katika miezi mitatu iliyopita, zote zikiwa za Ligi ya Mabingwa. Tunafungua ukurasa mpya na kusonga mbele. Hii ni Ligi ya Mabingwa, tunapaswa kuwapa wapinzani wetu sifa kwa walichokifanya.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.