Ripoti kutoka Italia zinadai kuwa kiungo wa Juventus, Weston McKennie amekataa ofa kutoka kwa Bournemouth, lakini angependelea kujiunga na Chelsea, Tottenham au Borussia Dortmund.

Mchezaji huyo wa Kimataifa wa USMNT ni mmoja wa wachezaji ambao wanaweza kuondoka Turin katika dirisha la usajili la Januari kwa ofa nzuri itakayoletwa.
Mchezaji huyo wa zamani wa Schalke anapatikana kwa €30-40m na Il Corriere dello Sport na Tuttosport zinadai kuwa Bournemouth ya Ligi Kuu ya Uingereza itakuwa tayari kutimiza matakwa ya Bianconeri.
Hata hivyo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 hana nia ya kujiunga na timu hiyo ya Ligi Kuu, hivyo klabu hizo mbili hazitarajiwi kusonga mbele kwa mazungumzo.

McKennie angependa kuhamia Ligi ya Primia, lakini ikiwa tu atapokea ofa kutoka kwa klabu kubwa zaidi, kama vile Chelsea au Tottenham, ripoti Il Corriere dello Sport.
Borussia Dortmund pia ni chaguo kwa kiungo wa kati wa Marekani aliyecheza Bundesliga kabla ya kujiunga na Juventus kwa mkataba wa mkopo wa awali mnamo 2020.

Miamba hao wa Serie A waliweka uhamisho wake wa kudumu kwa €18.5m mwaka 2021 na McKennie amefunga mabao 13 katika mechi 91 akiwa na Juventus.

