Pedri tayari ni mmoja wa wachezaji bora duniani katika nafasi yake, kwa mujibu wa kocha wa Barcelona Xavi.

Kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 20 alicheza mechi yake ya 100 kwa klabu hiyo jana akiwa na bao pekee wakati Barca wakiishinda Girona na kuambulia ushindi wa nane katika michezo tisa ya LaLiga.
Matokeo hayo yameifanya Barca kuwa mbele kwa pointi sita kwenye kilele cha ligi, ingawa Real Madrid wanaweza kupunguza pointi hadi tatu watakapoikaribisha Real Sociedad iliyo nambari tatu.
Xavi amesema kuwa; “Tayari ni mleta tofauti mkubwa kwenye michezo na ukiongeza pasi za mabao na mabao, tunazungumza juu ya mmoja wa wachezaji bora zaidi ulimwenguni katika nafasi yake akiwa na umri wa miaka 20 tu.”

Barca walikuwa mbali na ubora wao dhidi ya Girona, ambao sasa wameshindwa kushinda mechi yoyote kati ya tano za LaLiga dhidi ya Blaugrana, na Xavi anataka wachezaji wake wawe wajasiri zaidi katika hali ya kushambulia.
“Girona walitupa shinikizo na walitushangaza, lakini wakati mwingine tunahitaji kutoka nje ya boksi na kuzalisha zaidi. Kipindi cha kwanza cha nusu saa ya kipindi cha pili ndicho tunachotaka; ushindi na bao huja kutokana na presha kubwa.”

Pedri alichukua nafasi ya Ousmane Dembele aliyeumia dakika ya 26 na Xavi alithibitisha kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa atapimwa ili kubaini uzito wa suala hilo. Katika mechi kama hii ni muhimu zaidi kutompoteza Dembele kwani ndiye mchezaji muhimu zaidi katika hali ya mtu mmoja mmoja na, bila shaka, ilivuruga mipango yao.

