Klabu ya Ac Milan imeendelea kua na wakati mgumu katika ligi kuu ya Italia baada ya kupokea kichapo kizito katika mchezo wa ligi kuu nchini humo dhidi ya klabu ya Sassuolo.
Klabu ya Ac Milan leo imepokea kipigo cha mabao matano kwa mawili wakiwa ugenini wakikipiga na klabu ya Sassuolo katika mchezo wao wa 20 wa ligi kuu ya soka nchini Italia, Mabingwa hao watetezi wa ligi wameendelea kua na kiwango kibovu tangu kutoka kwenye michuano ya kombe la dunia.
Klabu hiyo chini ya kocha Stefano Pioli imekua ikipokea vipigo vizito siku za hivi karibuni kwani siku za hivi karibuni kwani katika mchezo uliopita walipokea kipigo cha mabao manne kwa bila dhidi ya klabu ya Lazio, Hivo na leo wameendelea na utaratibu wa kupokea vipigo vizito.
Klabu ya Ac Milan sasa imeweza kufikia rekodi yao mbovu ya msimu wa mwaka 2018 chini ya kocha Gattuso ambapo walicheza michezo sita bila kupata matokeo ya ushindi. Milan baada ya michuano ya kombe la dunia na kurejea kwa ligi mbalimbali wamecheza michezo sita mfululizo bila kupata matokeo ya ushindi.
Baada ya kupoteza mchezo wa leo klabu ya Ac Milan imeshuka mpaka nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya Italia kutoka nafasi ya pili kwenye msimamo, Klabu hiyo ambayo ndio mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Italia wanaonekana kuaga mapema sana mbio za ubingwa nchini humo kutokana na matokeo wanayoyapata hivi karibuni.

