Hakuna atakayebisha katika historia ya soka juu ya uwezo wa Cristiano Ronaldo ambaye amekuwa mchezaji bora wa wakati wote ndani ya kikosi chake cha timu ya taifa na katika klabu nyingi alizokwisha kuzichezea. Mbali na kuwa ni mchezaji hatari pia ni kiongozi mhamasishaji ndani ya timu yake na kuona kwamba kwa hayo aliyonayo hafananishwi na yeyote kwa uwezo wake ndani na maisha yake nje ya uwanja.
Kuna kizazi ambacho kimeamza kutabiriwa mema kwamba kinaweza kuwa bora kuleta ushindani na kujaribu kufikia pale ambapo mtangulizi wao ameweza kupafikia kwa wakati uliopo; jambo ambalo litaendelea kuchagiza ushindani katika soka. Baadhi ya majina yanayohusishwa ni;
Kylian Mbappe
Katika umri wake amekuwa tayari ni taa ya mafanikio ndani ya taifa lake na klabu anayoichezea pia. Ameweza kuwa mchezaji bora wa dunia katika miaka ambayo wengi huanza kuwa chipukizi na kuanza kujulikana kama wapo katika ulimwengu huo wa soka. Anapewa nafasi kubwa ya kuvaa viatu vya Ronaldo na Messi kutokana na kuanza kuzivunja rekodi zake mapema sana kwenye maisha yake ya soka la ushindani.
Anthony Martial
Mchezaji huyo wa United anaonekana kufuata nyayo zake za kisoka kutokana na kile anachokifanya akiwa uwanjani. Ni mwenye uwezo wa pekee sana ambao unafanya watu wazungumzie hatma ya uwezo wake kwamba atakuja kuwa tishio zaidi kutokana na umri wake kumruhusu kufanya hivyo. Katika msimu wake huu amecheza mechi 28 akifunga magoli 11 na kutoa pasi za magoli mbili kitu ambacho ni cha ubora mkubwa japo kwa sasa anakumbana na kipindi kigumu cha kurejesha afya yake.
Joao Filipe
Sio jina linalofahamika sana katika ulimwengu wa soka lakini mchezaji huyo ndiye aliyeweza kukuzwa kutoka chuo cha kufunzia wachezaji cha Benfica na kwa sasa ameweza kupandishwa kuchezea timu ya wakubwa. Uwezo wake sio kitu cha kubeza na ana kipaji cha pekee sana ambacho kinamfanya kuwa bora zaidi. Amejenga heshima kwa kushinda Euro zake za vijana chini ya miaka 19 na ile ya miaka chini ya 17.
Mason Greenwood
United wana bahati sana na historia ya kutambua wachezaji ambao huwa na uwezo wa pekee kwenye soka. Raia huyo wa Uingereza amekuwa na kipindi kizuri ndani ya kikosi hicho pekee cha United kutokana na takwimu zake ambapo katika michezo 22 amefunga magoli 22 na kutengeneza mengine sita. Anaonekana kuja kuwa Ronaldo mwingine.
Tuwape muda zaidi.


aisha
ama kweli pongezi nyingi ziende kwa Ronaldo
Furahav
Hatotokea km ronakdo duniani
Zeiyana
Utakua mfano tu na sio lonaldo wenyew alisia lonaldo hatabaki kama lonaldo
Evaluziga
Hakuna Kama Ronaldo
Povel
Cr7 mnyama sana