Simba kamili kuwamaliza Namungo usiku wa leo

JUMA Mgunda, kocha msaidizi wa Simba amesema maandalizi yote kwa ajili ya mchezo mgumu dhidi ya Namungo yamekamilika.

Timu hii inatarajiwa kumenyana na Namungo kwenye mchezo wa mzunguko wa pili Uwanja wa Majaliwa saa 1:00 usiku.

Ikumbukwe kwamba mchezo uliopita kwa Namungo walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City na kwa upande wa Simba ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Yanga mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Simba kamili kuwamaliza Namungo usiku wa leo

Vinara wa ligi ni Yanga wenye pointi 68 baada ya kucheza mechi 26. Namungo ina pointi 35 ipo nafasi ya 6 huku Simba ikiwa ina pointi 63 nafasi ya pili msimamo wa ligi.

Mei 2 Simba ilifanya mazoezi ya mwisho Uwanja wa Majaliwa na miongoni mwa mastaa waliokuwa kwenye mazoezi ni pamoja a Augustino Okra, Jonas Mkude, Clatous Chama.

Simba kamili kuwamaliza Namungo usiku wa leo

Mgunda amesema:”Maandalizi yote ya mchezo mgumu dhidi ya Namungo yamekamilika wachezaji wanatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu na wenye ushindani.

“Ratiba ilikuwa inajulikana tangu awali kabla ya kwenda Morocco hivyo tumerejea kwa ajili ya kuendelea kile ambacho kilikuwa kimepangwa na nguvu zetu zitakuwa kwenye mashindano ambayo tunashiriki,”.

Acha ujumbe