Beki wa zamani wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Uingereza Rio Ferdinand amefanikiwa kujumuishwa kwenye kikosi cha heshima cha ligi kuu ya Uingereza maarufu kama Premier League Hall of Fame.
Rio Ferdinand aliingia kwenye kinyang’anyiro hicho wiki kadhaa nyuma akiwa na magwiji wengine kama Nemanja Vidic, na Tony Adams lakini mpaka sasa gwiji huyo wa zamani wa Man United ameteuliwa pamoja na nahodha wa Arsenal Tony Adams ndio wamefanikiwa kupewa heshima hiyo.
Premier League Hall of Fame imekua na lengo la kuwapa heshima magwiji ambao wameitumikia ligi hiyo kwa mafanikio makubwa na mpaka sasa magwiji wengi wameshapewa heshima ya kujumuishwa kwenye kikosi hicho, Lakini mchakato bado unaendelea wa kuendelea kuwachagua magwiji hao kujumuika na wengine.
Rio Ferdinand amekua na mafanikio makubwa ndani ya klabu ya Manchester United haswa kwenye ligi kuu ya Uingereza akifanikiwa kuisaidia klabu huyo kutwaa mnataji sita ya ligi kuu ya Uingereza kwa vipindi tofauti tofauti, Vilevile akiwa na rekodi nzuri kama mlinzi ndani ya klabu hiyo.
Baada ya Rio Ferdinand kujumuishwa kwenye kikosi cha heshima cha ligi kuu ya Uingereza watu wengi wamempongeza beki huyo, Lakini wengi wakisubiri kuona pia beki mwenzake waliocheza nae kwa mafanikio ndani ya timu hiyo Nemanja Vidic akijumuishwa na yeye akijumuishwa kwenye timu hiyo kutokana na ubora ambao alikua nao.

