Staa wa klabu ya PSG Lionel Messi taarifa zinaeleza ataondoka ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu huku akihushwa na kurejea ndani yake ya zamani klabu ya Barcelona.
Messi inaelezwa hana furaha ndani ya klabu ya PSG na ndio chanzo cha mchezaji huyo kutimka ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu, Barcelona wanahusishwa zaidi kumrejesha klabuni hapo lakini vilevile vilabu mbalimbali kutoka Uarabuni vinahitaji saini yake.
Mchezaji huyo wa dunia mara saba amekua na msimu mzuri sana ndani ya PSG pamoja na timu ya taifa ya Argentina baada ya kushinda kombe la dunia, Lakini amekua hafurahishwi kuwepo ndani ya viunga vya Parc de Princess kutokana na kuhisi hapewi heshima ambayo anaistahili ndani ya timu hiyo.
Siku moja iliyopita taarifa kutoka ndani ya klabu ya PSG inaeleza Messi atapewa adhabu kutokana na kuondoka timu na kwenda Saudia Arabia bila ruhusa, Hii inaendelea kuchochea uwezekano kwa gwiji huyo kutimka ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Messi licha ya kuelezwa kua anaondoka ndani ya PSG mwishoni mwa msimu huu lakini bado hakuna uhakika wa klabu ambayo inatajwa kua na uhakika wa kunasa saini ya staa huyo wa zamani wa Barcelona, Lakini Barca wanapewa nafasi kubwa zaidi ya kuweza kumsainisha gwiji kurejea kwenye viunga vya Camp Nou.

