Simba Yaifuata Namungo Lindi

Klabu ya Simba imeanza safari hii leo ya kuifuata Namungo FC kwaajili ya mchezo wao wa ligi kuu ya NBC ambao unatarajiwa kupigwa siku ya Jumatano katika dimba la Majaliwa.

 

Simba Yaifuata Namungo Lindi

Simba sasa baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, wamebakiza matumaini ya kupata Makombe mawili wakiyapigania ambayo ni kombe la Ligi na Kombe la Shirikisho la Azam ambalo wapo nusu fainali.

Wekundu wa Msimbazi ambao wapo chini ya kocha mkuu Robertinho wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi zao 63 baada ya kucheza michezo 26 huku kinara wa ligi Yanga akiwa na pointi zake 68.

Namungo FC yeye anashikilia nafasi ya 6 akiwa na pointi zake 35 huku akiwa ameshinda michezo 10 sare 5 na kupoteza 11 huku mcehi ya mwisho akiwa ameshinda.

Simba Yaifuata Namungo Lindi

Namungo FC toka apande ligi kuu hajawahi kumfunga mnyama, na mechi ijayo anahitaji pointi 3. Je ataweza mbele ya Wekundu hao ambao wanahitaji kugombania ligi kuu?. Mara ya mwisho kukutana mnyama aliondoka na ushindi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.