Simba Yaondolewa Kibishi Ligi ya Mabingwa

Klabu ya Simba imeondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika na Wydad Casablanca baada ya wachezaji wao wawili Shomari Kapombe na Cloutus Chama kukosa mikwaju ya penalti 4-3.

 

Simba Yaondolewa Kibishi Ligi ya Mabingwa

Mchezo wa jana ulipelekea Simba na Wydad kwenda hatua ya mikwaju ya penati baada ya kufungwa bao 1-0 wakiwa ugenini dakika ya 24 ya mchezo na kufanya aggregate kuwa ni 1 kwa 1 baada ya mnyama kushinda bao moja nyumbani.

Timu zote mbili zilikuwa zikicheza kwa presha hasa kipindi cha kwanza cha mchezo ambacho mwisho kikapeleka Simba kufanya makosa na kufungwa bao mapema kipindi cha kwanza cha mchezo.

Licha ya ubora ambao mnyama ameuonyesha lakini hapo jana eneo la ushambuliaji halikufanya kazi nzuri na hivyo kumaliza mechi bila kuwa na shuti lolote ambalo limelenga lango mpaka mpira kumalizika.

Simba Yaondolewa Kibishi Ligi ya Mabingwa

Baada ya kutolewa kwenye ligi ya mabingwa sasa watarejea nyumbani kujipanga kwaajili ya makombe ambayo yamebaki ikiwemo ligi pamoja na Kombe la Shirikisho la Azam ambalo hatua ya nusu fainali watacheza dhidi ya Azam.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.