Ligi kuu ya NBC inaendelea hii leo kwa mchezo mmoja ambapo Mbeya City watawaalika Ruvu Shooting katika dimba lao la Sokoine majira ya saa 10:00 jioni.

Mbeya City wapo nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo yake 24, huku kwenye hiyo michezo aliyocheza ameshinda sita pekee, akienda sare michezo tisa, na kupoteza tisa akikusanya alama zake 27.
Huku vijana wa Mbwana Makata wao ndio vibonde wa ligi wakiwa wameshinda mechi zao nne pekee kwenye michezo yao 24, sare tano na kupoteza mara 15 huku ikiwa ni idadi kubwa ya mechi walizopoteza kuliko timu yoyote.

Mbeya City wametoka kushinda mechi yao iliyopita, huku Ruvu wao wakipoteza mechi yao iliyopita kwenye ligi. Matumaini ya kubakia ligi kuu yanazidi kufifia kwao hadi sasa.
Mechi ya mwisho kukutana timu hizi mbili, Wanakoma Kumwanya waliondoka na pointi tatu. Je leo hii mgeni anaweza kulipa kisasi kwa kupata ushindi? ODDS KUBWA unazipata mechi hii ndani ya Meridianbet.

