Geita Gold FC licha ya kuondokewa na wachezaji zaidi ya watano (5) wakati wa dirisha dogo la usajili, tena wengi wakiwa wa kikosi cha kwanza bado imeweza kufanya vizuri katika mechi zake tatu (3) baada ya usajili wa dirisha dogo.
Baadhi ya wachezaji walioondoka katika timu hiyo ni Said Ntibazonkiza, Yusuph Kagoma, Kelvin Nashon, Adeyum Saleh, Yahya Mbegu, Juma Mahadhi, Miraj Athumani, Ramadhan Chombo ‘Redondo’.
Katika mechi tatu (3) ilizocheza bila nyota wengi waliotimkia timu nyingine, timu hiyo imeshinda mechi mbili (2) na kutoka sare mchezo mmoja (1).
▪️Geita Gold 1-0 Coastal Union
▪️Geita Gold 1-1 Polisi Tanzania
▪️Geita Gold 2-0 Dodoma Jiji
Baada ya mchezo wa jana dhidi ya Coastal Union, timu hii imefikisha alama 31 huku ikiwa nafasi ya tano (5) kwenye msimamo wa Ligi mahali ambako hakuna presha ya kushuka daraja.
Hiyo ni kazi nzuri ya Kocha Mkuu Fred Felix Minziro ‘Baba Isaya’ ambaye ni beki wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, yeye na benchi lake la ufundi, licha ya kikosi chake kutikiswa kwa kuondoka wachezaji wengi bado kinapiga kazi bomba.