Manchester United Kukipiga Nusu Fainali ya Carabao Leo

Klabu ya Manchester United leo itashuka dimbani kumenyana na klabu ya Nottingham Forest kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la Carabao nchini Uingereza.

Manchester United leo itasafiri mpaka jiji la Nottingham kwenda kukipiga na klabu ya ya Nottingham Forest katika dimba la City Ground, Mchezo huo unaweza kuipa klabu hiyo ya kucheza fainali na kushinda kikombe cha kwanza ndani ya msimu huu.manchester unitedKlabu ya Manchester United haijafanikiwa kubeba taji lolote kuanzia mwaka 2017 waliposhinda taji la Europa chini ya kocha Jose Mourinho, Hivo klabu hiyo ipo kwenye mpango wa kuhakikisha wanarudisha heshima ya timu hiyo iliyopotea kwa muda mrefu na ili kurudisha heshima basi wanahitaji kushinda mataji.

Man United chini ya kocha ,pya wa klabu hiyo Erik Ten Hag wamekua kwenye mwenendo mzuri na kufanikiwa kuirudisha klabu hiyo kwenye nafasi nne za juu mpaka sasa, Huku akiwa katika nsu fainali ya kombe la Carabao ambapo wanaweza kufuzu hatua ya fainali pia.manchester unitedKlabu ya Manchester United ndio klabu pekee kutoka nchini Uingereza ambayo imebaki kwenye michuano yote msimu huu, Man United ipo kwenye kombe la Europa, Carabao, kombe la Fa, pamoja na kombe la ligi kuu ya Uingereza na hii inaonesha kua klabu hiyo ipo kwenye mwelekea mzuri.

Acha ujumbe