Klabu ya Manchester United itashuka dimbani leo kumenyana na klabu ya Crystal Palace ambao watakua nyumbani katika dimba lao la Selhurst Park usiku wa leo.
Manchester United leo watakua ugenini leo kumenyana na klabu ya Crystal Palace katik mchezo wa ligi kuu ya Uingereza. Mchezo huo ambao utatoa taswira ya ubingwa kwa klabu hiyo kama itafanikiwa kushinda mchezo huo.
Klabu hiyo endapo itafanikiwa kushinda mchezo wa leo dhidi ya Crystal Palace watakua wamebakiza alama sita ili kuweza kuwafikia vinara wa ligu ya Uingereza klabu ya Arsenal ambayo watakwenda kumenyana nayo wikiendi inayofuata katika dimba la Emirates.
Klabu ya Manchester United imefanikiwa kushinda michezo tisa mfululizo kwenye michuano yote mpaka wakati huu, Huku wakifanikiwa kushinda michezo sita ya ligi kuu ya Uingereza mfululizo hivo watakwenda kwenye mchezo huu wakiwa na moto uleule ambao wamekua nao hivi karibuni.
Klabu ya Crystal Palace imekua na mfululizo wa matokeo mabaya kwa siku za hivi karibuni katika michezo yao minne ya mwisho ya ligi kuu ya Uingereza wamefanikiwa kushinda mchezo mmoja na kufungwa michezo mitatu, Hivo klabu hiyo inaweza kubadilika kwenye mchezo huo dhidi ya Manchester United kwenye dimba lao la nyumbani.

