Jack Grealish anasisitiza kuwa Kocha mkuu wa Uingereza Gareth Southgate hana tatizo na kiungo yeyote wa kikosi cha Uingereza alipokuwa akijibu madai yaliyotolewa na beki wa zamani Gary Neville.

Kocha wa Uingereza Southgate alikosolewa na wengi, akiwemo Neville, kwa kutomchezesha kiungo Phil Foden wakati wa sare ya bila kufungana ya Kombe la Dunia Ijumaa dhidi ya Marekani.
Akizungumza katika nafasi yake kama mchambuzi Neville alicheza mara 85 na Uingereza na alisema kuwa; “Phil Foden ni kipaji cha kizazi ambacho ninahisi kama anapaswa kucheza, lazima achzeshwe kwa fomu yake na lazima afanye kazi na Uingereza. Nilipitia maisha yangu ya uchezaji Uingereza ambapo kuna wakati Paul Scholes alifanyiwa kazi vibaya.”
Hata hivyo, Grealish amekanusha kuwa Southgate ana matatizo na watu binafsi, kwa kuwa yeye mwenyewe amekuwa katika hali sawa na Foden kwenye Euro 2020 alipokuwa akihangaika.

Grealish aliendelea kusema kuwa kama angekuwa na tatizo wangejua akisema kuwa kuna kitu kinaendelea nyuma ya pazia, na watu siku zote walikuwa wakisema ana tatizo na Jack kama miaka miwili iliyopita.
Alisema kuwa kocha wao anazungumza nao wote sawa, na Foden hakucheza mechi lakini bado yupo sawa kama alivyo Harry Kane. Uingereza iliishinda Iran kwa mabao 6-2 na kuanza vyema kampeni za Kombe la Dunia kabla ya kupata sare na Marekani.
Kwa pointi nne kutoka kwenye mechi mbili, vijana wa Southgate watatinga hatua ya 16 bora ikiwa hawatapoteza mchezo wao wa leo dhidi ya Wales kwenye Uwanja wa Ahmed bin Ali.

Grealish ameongeza kwa kusema kuwa wakati mwingine anadhani chochote kitakachotokea Uingereza huwa kuna kitu. Walifunga sita na walikuwa kitu bora. Wako juu ya Kundi hilo, na hatma yao iko mikononi mwao.
Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.
BONYEZA HAPA KUCHEZA


