Shomari Kapombe beki wa Simba amesema kuwa walikutana na ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani wao TMA Stars katika mchezo wa hatua ya 32 bora CRDB Federation Cup uliochezwa Uwanja wa KMC Complex.

Katika mchezo huo uliochezwa Machi 11 2025 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 3-0 TMA Stars kwa mabao ya Valentin Nouma dakika ya 15, Sixtus Sabilo alijifunga dakika ya 19 na Leonel Ateba alifunga bao la tatu dakika ya 75.
Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.
Kwenye mchezo huo nyota Sabilo dakika ya 45 alifanya jaribio la hatari ambalo lilimpa tabu kipa namba mbili wa Simba, Ally Salim ambaye alikuwa langoni kwenye mchezo huo likiwa ni jaribio pekee lililokuwa na hatari zaidi kwa upande wa TMA Stars.


