Klabu ya Al-Hilal ya Saudia Wamemnasa Beki wa Chelsea Koulibaly

Kalidou Koulibaly amekuwa mchezaji nyota mwingine zaidi kuhamia katika ligi ya Saudi Arabia akitokea Chelsea.

 

Klabu ya Al-Hilal ya Saudia Wamemnasa Beki wa Chelsea Koulibaly

Al-Hilal wamekamilisha dili la kumnunua beki huyo wa Senegal, ambaye anamaliza muda wake Chelsea baada ya msimu mmoja pekee.

Taarifa kwenye tovuti rasmi ya klabu hiyo ya London ilisema: “Tungependa kumshukuru Kalidou kwa mchango wake ndani na nje ya uwanja wakati akiwa Stamford Bridge na tunamtakia kila la kheri kwa hatua inayofuata ya maisha yake ya soka.”

Chelsea walitumia kitita cha pauni milioni 33 kumnasa beki huyo wa kati kwa kandarasi ya miaka minne msimu uliopita wa joto lakini mchezaji huyo wa kimataifa aliyecheza mechi 70 alishindwa kutamba.

Klabu ya Al-Hilal ya Saudia Wamemnasa Beki wa Chelsea Koulibaly

Alicheza mechi 32 katika mashindano yote huku The Blues wakiporomoka hadi kumaliza katika nafasi ya 12 kwenye Ligi Kuu.

Koulibaly mwenye miaka 32, amemfuata mchezaji mwenzake wa zamani N’Golo Kante, ambaye alijiunga na Mfaransa mwenzake Karim Benzema katika klabu ya Al-Ittihad mapema mwezi huu, hadi Ligi Kuu ya Saudia.

Baada ya kutambulishwa na klabu yake mpya, mshindi huyo wa Kombe la Mataifa ya Afrika alisema: “Niko hapa na wale wanaofanya utukufu kwa sasa na siku zijazo.”

Acha ujumbe