Mourinho Anataka Roma Wamsajili Greenwood

Tetesi kutoka Uingereza zinadai kuwa Jose Mourinho amewasiliana na Mason Greenwood kujadili uwezekano wa kuhamia Roma kwa mkopo.

 

Mourinho Anataka Roma Wamsajili Greenwood

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 hajacheza hata dakika moja ya soka la kikosi cha kwanza tangu Januari 2022, aliposhutumiwa kwa ubakaji na unyanyasaji. Video na picha zilienea haraka kwenye mitandao ya kijamii na akatupwa na Mashetani Wekundu.

Mnamo Februari mwaka huu, mashtaka yaliondolewa dhidi ya Greenwood, lakini bado hajarejea uwanjani, ingawa alionekana akifanya mazoezi peke yake katika kituo cha michezo cha umma hivi karibuni.

Jarida la udaku la Uingereza The Sun linadai kuwa Mourinho hivi majuzi aliwasiliana na Greenwood ili kuchunguza uwezekano wa kuhamia Roma kwa mkopo.

Mourinho Anataka Roma Wamsajili Greenwood

Chanzo kinadaiwa kuliambia jarida hilo kwamba; “Jose alimpigia simu baba yake Mason na pia alizungumza na Mason. Alimwambia njia bora ya kutoka katika hali yake ya sasa ni kuanza kucheza soka na kwamba hatimaye matatizo yote yatatoweka.”

Kocha huyo wa Roma anamfahamu Greenwood vyema tangu walipokuwa pamoja Manchester United, baada ya kumtambua kama kipaji bora alipokuwa na umri wa miaka 15.

Mourinho Anataka Roma Wamsajili Greenwood

Mwingereza huyo bado ana kandarasi na Red Devils hadi Juni 2025 lakini kuna uwezekano mkubwa wa kurejea kwenye kikosi cha kwanza.

Acha ujumbe