Fikayo Tomori alitafakari juu ya kuondoka kwa Paolo Maldini Milan, akisema kuwa hakuna mtu mwingine kama yeye kwenye klabu.

 

Tomori: "Unapofikiria Milan, Unafikiria Maldini"

Mmiliki wa Rossoneri Gerry Cardinale aliamua kumfukuza mkurugenzi huyo wa ufundi mwanzoni mwa mwezi uliopita pamoja na mkurugenzi wa michezo Frederic Massara, kuashiria mabadiliko katika sera ya soko la uhamisho.


Milan wamemuuza Sandro Tonali kwa Newcastle United na kuwasajili Ruben Loftus-Cheek na Christian Pulisic kutoka Chelsea.

Akizungumza na Sky Sports Italia kupitia Di Marzio, Tomori alitazamia kwa mara ya kwanza msimu ujao wa 2023-24.

Tomori: "Unapofikiria Milan, Unafikiria Maldini"

“Tuna furaha na msisimko. Huu ni msimu wangu wa tatu na nafasi yangu uwanjani inanihitaji kuwa kiongozi, niwe mtu wa kuzungumza mengi ndani na nje ya uwanja. Mimi karibu ni mkongwe, nimefika miaka mitatu na nusu iliyopita. Ninahisi jukumu, kama kila mtu mwingine, kwa sababu tunataka kushinda.”

Alitafakari ni wapi mambo yalienda vibaya kwa Milan msimu uliopita na nini kinaweza kuwa tofauti katika kampeni ijayo.

Tomori amesema kuwa, mwaka jana walikuwa na mwezi wa Januari ambao uliharibu msimu, isipokuwa katika Ligi ya Mabingwa. Anatumai mwaka huu watakuwa bora, wanataka kushinda lakini wanajua itakuwa ngumu zaidi.

Tomori: "Unapofikiria Milan, Unafikiria Maldini"

“Tunajaribu mambo tofauti na kocha, tunajivunia kuwa wachezaji wa Milan na tunataka kuthibitisha hilo uwanjani. Natumai utakuwa msimu wa kukumbuka.”

Hatimaye, Tomori alitafakari kuhusu uhusiano wake na Maldini na uamuzi wa klabu kumfuta kazi mwezi uliopita.

Alisema kuwa unapofikiria Milan, unafikiria Maldini. Alipofika, alimwona kila siku huko Milanello, na alimpa ushauri jinsi ya kuwa na nguvu zaidi. Hakuna mtu mwingine kama yeye, lakini klabu imeamua kubadilika na wao kama wachezaji wanalenga uwanjani.

Tomori: "Unapofikiria Milan, Unafikiria Maldini"

Tomori alikuwa mmoja wa wachezaji wengi walioletwa Milan na Maldini na amekua mtu muhimu kwenye klabu, na kucheza mechi 107 katika mashindano yote tangu kuwasili kwake kwa mara ya kwanza mnamo Januari 2021.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa