Mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea Fikayo Tomori leo atarejea nyumbani katika mchezo wa ligi ya mabingwa utakaozikutanisha klabu za Chelsea wakiwa nyumbani dhidi ya Ac Milan.
Mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Stamford Bridge utamrudisha nyumbani kwa mara ya kwanza Fikayo Tomori wakati akiondoka klabuni hapo kama kijana sasa anarudi kama mwanaume na mabingwa wa soka nchini Italia klabu ya Ac Milan.
Mchezaji huyo ambaye amekua katika akademi ya klabu ya Chelsea alitolewa kwa mkopo kuelekea Ac Milan mwaka 2021 kabla ya kuuzwa jumla klabuni hapo mwaka huohuo.
Fikayo Tomori amekua mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Ac Milan chini ya mwalimu Stefano Pioli baada ya kutumika zaidi katika msimu wa 2021/22 ambapo klabu hiyo walifanikiwa kua mabingwa wa Italia na kuendelea kua mchezaji muhimu kikosini.
Mbali na Tomori Olivier Giroud nae atarudi kwenye klabu yake ya zamani ya Chelsea aliyopata mafanikio nayo kwa kubeba mataji kadhaa kama Ligi ya mabingwa ulaya mwaka 2021 na Uefa Europa League.